IQNA

Msichana aliye na umri wa miaka 10 kuiwakilisha Iran mashindano ya Qur'ani ya UAE

22:10 - September 29, 2017
Habari ID: 3471198
TEHRAN (IQNA)-Msichana mwenye umri wa miaka 10 ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Shaikha Fatima Bint Mubarak ya Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Zahra Sadat Husseini mwenye umri wa miaka 10 ameteuliwa kutoka miongoni mwa wasichana wengine saba ambao ujuzi na ustadi wao katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ulitathminiwa na jopo la wataalamu Wairani.

Jopo hilo lilimteua Zahra Husseini kutoka mkoa wa Khorassan Razavi kaskazini mashariki mwa Iran baada ya kupata pointi nyingi Zaidi miongoni mwa wasichana wenzake na hivyo kupata fursa ya kuiwakilisha Iran katika mashindano hayo ya kimataifa ambaye washiriki wake ni wanawake wenye umri usiozidi miaka 25.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Shaikha Fatima Bint Mubarak ya UAE yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu. Mwaka jana washiriki sabini kutoka nchi mbali mbali walishindani kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika mashindano hayo yaliyofanyika Novemba 6-18 mwaka 2016.

Mwaka jana Iran iliwakilishwa na Hannaneh Khalafi ambapo nafasi ya kwanza ilishikwa kwa pamoja na Zahra Hani from Algeria and Zakiya Abu Bakr Mahmoud Ilmi wa msumbiji.Msichana aliye na umri wa miaka 10 kuiwakilisha Iran mashindano ya Qur'ani ya UAE

Hannaneh Khalafi, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka tisa, alishika nafasi ya 10 kwa pamoja na Amina Jafar wa Nigeria. Hannaneh, ambaye alitajwa na televisheni ya Misri kuwa ‘kompyuta’ kutokana na ustadi wake katika kujibu maswali ya kuhifadhi Qur’ani, alikuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi katika mashindano hayo ya Dubai.

Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya Qur’ani yajulikanayo kama Zwadi ya Kimatiafa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3647294

captcha