IQNA

Msikiti Scotland wahujumiwa kwa maandishi ya kibaguzi

15:00 - May 23, 2019
Habari ID: 3471969
TEHRAN (IQNA) - Polisi katika jimbo la Scoltand nchini Uingereza wanachunguza kitendo cha uhalifu cha chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) baada ya maandishi dhidi ya Waislamu kupatikana yameandikwa katika kuta za msikiti eneo hilo.

Taarifa zinasema tukio hilo lilijiri Jumatatu usiku katika Kituo cha Kiislamu cha Elgin kaskazini mwa Scotland ambapo nembo ya kinazi ya Swastika ilichorwa katika kuta za misikiti mbali na maandishi mengine ya matusi na kibaguzi. Polisi Scotland wamesema tukio hilo halikubaliki hata kidogo.

Mkurugenzi wa Msikiti wa Elgin Lansana Bangura amesema wanawasiwsi mkubwa kufuatia tukio hilo huku akiongeza kuwa wamekuwa wakitarajia vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu. Aidha amesema vitendo kama hivyo havitavunja umoja uliopo baina ya jamii ya Waislamu Scotland na majirani zao huku akisema kuwa wasiokuwa Waislamu wamefungamna nao baada ya tukio hilo.

Afisa wa Idara ya Upelelezi Scotland Inspekta Martin MacDougall amesema hawatastahamili vitendo cha chuki dhidi ya Uislamu na kuongeza kuwa uchunguzi utafanyika kubaini wahusika. Pia amewahakikishia Waislamu kuwa kuwa doria zitaimarishwa katika eneo la msikiti.

3468584

 

captcha