IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Watawala wa Bahrain na Saudi Arabia wamefanya hiana kwa Palestina, wanaelekea katika kinamsi

17:09 - June 05, 2019
Habari ID: 3471987
TEHRAN (IQNA)- Kiingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu suala la Palestina na njama za uhaini za Marekani kupitia mpango wake wa 'Muamala wa Karne' ni kadhia ya kwanza kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo mjini Tehran katika hotuba za swala ya Idul-Fitri iliyosaliwa katika uwanja wa sala wa Imam Khomeini MA.

Sambamba na kusisitiza kwamba mpango unaoitwa 'Muamala wa Karne' hautofikia malengo yake, Kiongozi Muadhamu amepongeza nchi za Kiarabu na kadhalika makundi ya Palestina yaliyopinga mpango huo.

Amesema kuwa baadhi ya nchi za Kiislamu kama vile Bahrain na Saudi Arabia zimefanya hiana kutokana na kuhusika na uandaaji wa mpango huo mchafu. Kiongozi Muadhamu ameashiria uenyeji wa Bahrain kwa mkutano wa kiuchumi wa mpango wa Muamala wa Karne na kusema kuwa mkutano huo uliitishwa na Wamarekani, lakini viongozi wa Manama kwa udhaifu na kutokana na roho mbaya dhidi wananchi na dhidi ya Uislamu wamekubali kuwa wenyeji wake. Amesisitiza kwamba watawala wa Bahrain na Saudia lazima wafahamu kwamba, mienendo yao hiyo itaishia kukwama katika kinamasi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewashukuru pia raia wa Iran kutokana na kushiriki kwao kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kuongeza kwamba, ushiriki huo mkubwa na imara wa wananchi katika harakati hiyo, umekuwa na taathira katika siasa za dunia na kuwakatisha tamaa maadui wa taifa la Iran sambamba na kutia dosari mahesabu yao. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria pia baadhi ya ada nzuri  na za kuvutia za Kiislamu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani likiwemo suala la kusaidiana ambalo limestawi nchini hapa, na kusifu ushiriki wa wananchi kwa ajili ya kusaidia kutoa futari katika misikiti, husseiniya na maeneo ya kijamii, kama ambavyo pia ametaka kusaidiwa waathirika wa mafuriko ya hivi karibuni nchini. Ibada ya swala ya Idil Fitri mjini Tehran imeongozwa na Kiongozi Muadhamu. Waislamu wa Iran asubuhi ya leo wameshiriki ibada hiyo katika maeneo yote ya nchi hii baada ya kumalizika mwezi Mtukufuu wa Ramadhani. Leo Jumatano ilikuwa Siku Kuu ya Idul Fitri katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingi duniani.

3817282

captcha