IQNA

Waumini 30,000 washiriki Swala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa + Video

21:57 - June 27, 2020
Habari ID: 3472903
TEHRAN (IQNA) –Zaidi ya Waislamu 30,000 wameshiriki katika Swala ya Ijumaa katika msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) huku wakizingatia kanuni za afya zilizowekwa na idara ya wakfu mjini humo kwa lengo la kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Sheikh Azzam Khatib, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wakfu ya Jordan mjini Quds amesema sheria kali za kiafya zimewekwa kutokana na ongezeko la idadi ya walioambukziwa COVID-19 mjini Quds na miji mingine ya Wapalestina.

Amesema wamechukua hatua hiyo ili wasilaumiwa kuhusika katika kueneza COVID-19 katika mji wa Quds ambao unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Msikiti wa Al Aqsa ulikuwa umefungwa kwa muda wa miezi miwili hadi Mei 25 ikiwa ni katika hatua za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

3907038

captcha