IQNA

Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran inafanyika kupitia Intaneti

19:22 - March 07, 2021
Habari ID: 3473711
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran inaendelea ambapo kuna washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani kutokana na janga la  COVID-19 au corona, yanafanyika kwa njia ya intaneti.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yana majaji 23 kutoka Iran na wengine saba kutoka Sudan, Lebanon, Indonesia, Syria, Tunisia na Jordan. Majaji hao ambao wote ni wataalamu wa Qur’ani watasimamia zoezi zima la kusoma na kuhifadhi Qur’ani katika mashindano hayo.

Mtaalamu mkongwe wa Qur’ani kutoka Iran, Ustadh Abbas Salimi anaongoza jopo hilo la majaji katika mashindano hayo ambayo yameanza Machi sita na yanatazamiwa kumalizika Machi 11.

Mbali na kufanyika kwa njia ya intaneti, mashindano hayo pia yanarushwa hewani mubashara kupitia Televisheni ya Qur'ani ya IRIB, Radio ya Qur'ani ya IRIB na majukwaa mengine ya mtandaoni.

Mbali na kufanyika kwa njia ya intaneti, mashindano hayo pia yanarushwa hewani mubashara kupitia Televisheni ya Qur'ani ya IRIB, Radio ya Qur'ani ya IRIB na majukwaa mengine ya mtandaoni.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni 'Kitabu Kimoja, Ummah Mmoja".

Iran Int’l Quran Contest: Final Round Gets Underway

Zaidi watazamaji milioni 2.5 walifuatilia duru za mchujo za mashindano hayo kwa njia ya intaneti na inatazamiwa kuwa baina ya watu milioni 6-8 watafuatilia fainali ya mashindano hayo kwa njia ya intaneti.

Nusu fainali ya mashindano hayo ilifanyika mapema mwezi Februari njia ya intaneti ambapo kulikuwa na washiriki 120 kutoka nchi 70. Duru za awali za mchujo katika mashindano hayo zilikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70 na zilifanyika pia kwa njia ya intaneti kutokana na janga la corona. Washiriki 57 kutoka nchi 26 watashindano katika fainali za mashindano yam waka huu.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwisho Aprili 2019 mjini Tehran ambapo washiriki kutoka nchi zaidi ya 80 walishiriki.

3957979

captcha