IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya 'Aisha Sururu Foundation' yafanyika Tanzania

12:09 - April 22, 2021
Habari ID: 3473841
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu yamefanyika nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefanyika Aprili 18 mjini Dar-es-Salaam  na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya washiriki.

Mashidano hayo yametumika pia kumtafuta mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Qur'ani katika ngazi za kimataifa.

Mashindano hayo pia yalkuwa na kitengo maalumu cha wenye ulemavu wa macho.

Mashindano hayo yamehudhuriwa na wageni mbali mbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Iran nchini Tanzania Morteza Pirani.

Bi. Aisha Sururu ni mwanamke pekee barani Afrika anayeandaa Mashindano ya Qur'ani Tukufu na amekuwa akiandaa mashindano hayo kwa muda wa miaka 19 sasa.

3966001

captcha