IQNA

Jeshi la Yemen lamuangamiza kinara wa mgaidi wa Daesh na mamluki Saudia huko Ma’rib

19:44 - May 02, 2021
Habari ID: 3473870
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Yemen limefanikiwa kumuua kinara wa magaidi wa Daesh ambaye pia ni muitifaki mkubwa wa muungano vamizi wa Saudia katika mkoa wa Ma’rib.

Kinara huyo wa magaidi ametambuliwa kuwa ni Saleh Dirham Ramadi wa Brigedi ya 129 ya wanamgambo ambao wamekuwa wakiusaidia muungano vamizi wa Saudia tokea uanzishe vita vyake dhidi ya taifa la Yemen mwaka 2015.

Magaidi wakufurishaji wa makundi ya ISIS au Daesh pamoja na Al Qaeda wamekuwa wakijaribu kuimarisha satwa na ushawishi wao katika mkoa wa Ma’rib

Tarehe 26 Machi 2015, Saudi Arabia kwa msaada wa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na baadhi ya nchi za Ulaya na Kiarabu kama Uingereza na Sudan, ilianzisha mashambulizi ya kivamizi ya pande zote dhidi ya taifa maskini la Kiarabu na Kiislamu la Yemen. Muungano huo wa Saudia pia umekuwa ukishirikiana kwa karibu na makundi ya kigaidi katika vita vyake hivyo dhidi ya Yemen.

Wavamizi hao walikuwa na ndoto ya kuvimaliza vita hivyo katika kipindi cha wiki chache tu. Hata hivyo huu ni mwaka wa 7 na kadiri siku zinavyopita, ndivyo wananchi wa Yemen wanavyozidi kuwa imara katika muqawama na kujihami kwao kishujaa.

Yemen sasa inakabiliwa na maafa makubwa zaidi ya kibinadamu katika karne ya 21 ikiwa ni taathira ya vita ya vita hivyo vinavyoongozwa na Saudia dhidi ya nchi hii masikini zaidi katika bara Arabu.

3474599

Kishikizo: yemen MAARIB saudia
captcha