Shahid Qassem Suleimani aliuawa katika shambulio la kigaidi la anga la jeshi la Marekani Januari 3, 2020 huko Baghdad Iraq ambalo lilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.
Ebrahim Raisi amesema hayo Jumatano katika hotuba yake kwenye mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na ambapo pia amesisitiza kuweko uadilifu duniani na kubainisha kuwa, Iran inataka kuweko hatima na mustakabali wa pamoja kwa ajili ya mwanadamu na kwamba, inaunga mkono kuweko dunia yenye uadilifu ndani yake.
Rais wa Iran amesema hamu na shauku ya kutaka kuweko uadilifu ni adia ya Mwenyezi Mungu iko katika dhamira za wanadamu wote.
Rais wa Iran amesisitiza katika hotuba yake hiyo kwamba, Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran inaunga mkono kuweko dunia yenye uadilifu, kwani uadilifu unaleta umoja na kwamba, dhulma inachochea na kuleta vita na machafuko.
Rais wa Iran amesema katika sehemu nyingine ya hotuba yake hiyo kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa ni harakati ya wananchi wa Iran kuelekea ukweli na uhakika, ambapo licha ya kuweko fitina mbalimbali lakini yaliweza kulinda utukufu wa malengo yake.
Kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, Marekani ''ilikanyaga'' na kukiuka makubaliano hayo ya kimataifa yaliyosainiwa mwaka 2015, na kuongeza kuwa Iran haina nia ya kutengeneza silaha za atomiki kama ambavyo amesisitiza azma ya Tehran ya kuwa na uhusiano mwema na majirani zake wote.
3480586