IQNA

Rais Rouhani: Njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni mapambano

19:16 - May 25, 2021
Habari ID: 3473944
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa muqawama au mapambano ya mataifa dhidi ya wavamizi ndio njia pekee ya kuwashinda.

Rais wa Iran ameyasema hayo Jumanne katika ujumbe ambao amemtumia mwenzake wa Lebanon Michel Aoun kwa mnasaba wa ushindi wa taifa la Lebanon dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2000.

Amesema kukombolwa maeneo ya kusini mwa Lebanon ambayo yalikuwa yanakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel miaka 21 iliyopita ni ushindi uliojaa fakhari kwa taifa la Lebanon.

Rouhani amesema ushindi huo ulionyesha wazi kuwa njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni mataifa kusimama kidete na kupambana.

Rais Rouhani halikadhalika amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafungamana na taifa na serikali ya Lebanon katika kulinda umoja na mipaka ya nchi hiyo.

Kila mwaka mwezi Mei, Lebanon huadhimisha kumbukumbu ya kuondoka kwa  madhila wanajeshi vamizi wa Isrel katika ardhi zake za kusini. Siku hii nchini Lebanon hujulikana kama Siku ya Kitaifa ya Mapambano (Muqawama) na Ukombozi.

Itakumbukuwa kuwa, tarehe 25 Mei 2000, utawala wa Kizayuni licha ya kuwa na nguvu za kijeshi, ulisalimu amri mbele ya wanamapambano wa Kiislamu wa Lebanon na ulilazimika kukimbia kwa madhila kusini mwa nchi hiyo. Kila mwaka wananchi wa Lebanon wanaadhimisha siku hiyo ya kukimbia wanajeshi wa mwisho wa Israel kusini mwa nchi yao.

3973608

Kishikizo: iran rouhani lebanon israel
captcha