IQNA

Hamas, Jihad Islami zasisitiza haja ya mpango wa pamoja na PLO

14:10 - February 26, 2022
Habari ID: 3474978
TEHRAN (IQNA)- Harakati za Kiislamu za kupigania ukombozi wa Palestina, Hamas na Jihad Islami zimesisitiza ulazima wa kuafikiana na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kuhusu mpango wa pamoja wa kitaifa wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikoloni ardhi za Palestina.

Wajumbe kutoka Hamas na Jihad Islami walifanya mazungumzo huko Beirut, Lebanon, siku ya Ijumaa, tovuti ya Qudspress.com iliripoti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baadaye, pande hizo mbili zilisema zilijadili hali ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwenye mkutano huo.

Vile vile wamesisitiza uungaji mkono wao wa dhati kwa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni.

Walielezea kuendelea kwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, hususan al-Quds (Jerusalem), na kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kuwa ni jambo lisilovumilika.

Hamas na Jihad Islami wametoa wito wa umoja wa Wapalestina na makubaliano ya mpango wa pamoja wa kitaifa na PLO kukabiliana na utawala wa ghasibu wa Israel.

Pia walikariri kukataa kwao mpango wowote unaodhoofisha kadhia ya Palestina.

4038763

 

captcha