IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran husambaratisha propaganda za maadui

16:25 - March 05, 2022
Habari ID: 3475008
TEHRAN (IQNA) - Qari wa Qur'ani Tukufu wa Iran anayetambulika kimataifa alisisitiza umuhimu wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran katika kukabiliana na propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Abbas Emamjome amesema kuna mashambulizi mengi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na hasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na shughuli za Qur'ani.

Alisema maadui wakiwemo Mawahabi walieneza dhana potofu kwamba Waislamu wa madhehebu ya Shia hawaizingatii Qur'ani au kwamba Qur'ani yao ni tofauti na Waislamu wengine.

Wakati Iran inapoandaa tukio la Qur'ani kama mashindano ya kimataifa ya Qur'ani, mashambulizi kama hayo yanazuiwa na taarifa kama hizo za uwongo zinakanushwa, alisema.

Emamjome amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata maendeleo makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu katika masuala ya shughuli za Qur'ani.

Wakati mabingwa wakuu wa Qur'ani  wakiwemo wahifadhi na wasomaji wa Qur'ani wanakuja Iran kwa ajili ya mashindano hayo, wanajionea wenyewe, aliongeza.

Hatua ya mwisho ya mashindano ya 38 ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran, yaliyoanza Jumatatu, itakamilika kwa hafla ya Jumamosi jioni, ambapo washindi watatangazwa na kutunukiwa tuzo.

Jumla ya maqari 62 na wahifadhi kutoka nchi 29 wameshindana katika hatua hii ya hafla hiyo, ambayo inafanyika kwa karibu.

84670617

captcha