IQNA

Polisi wa Ufaransa Watumia Mabomu ya Machozi na Maji Kuzuia Maandamano Watu wanaounga Mkono Wapalestina

11:55 - October 14, 2023
Habari ID: 3477727
PARIS (IQNA) - Polisi mjini Paris walitumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kutawanya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina siku ya Alhamisi huku serikali ya Ufaransa ikipiga marufuku maandamano yanayoiunga mkono Palestina kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

 

Waandamanaji wa Ufaransa siku ya Alhamisi wamelaani utawala wa Israel kwa kuwaua raia huko Gaza na kumshutumu Rais Emmanuel Macron kwa kuegemea upande wa uvamizi huo.

Licha ya marufuku hiyo, mamia ya wanaharakati wanaounga mkono Palestina walikusanyika katikati mwa Paris, wakiimba muuaji wa Israel na mshirika wa Macron, Walikutana na polisi wa kutuliza ghasia ambao walijaribu kuwazuia kuungana kwa kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Waandamanaji hao walisema wana haki ya kueleza mshikamano wao na Wapalestina, ambao wamekuwa chini ya mashambulizi ya Israel kwa wiki moja, Pia walikosoa mamlaka ya Ufaransa kwa kuruhusu mikutano inayoiunga mkono Israel lakini sio ile inayoiunga mkono Palestina.

Tunaishi katika nchi ya sheria za kiraia, nchi ambayo tuna haki ya kuchukua msimamo na kuandamana, Si haki kukataza upande mmoja na kuidhinisha upande mwingine na hiyo haiakisi ukweli wa Palestina ,alisema Charlotte Vautier, 29, mfanyakazi katika shirika lisilo la faida.

Maandamano hayo ya mjini Paris yalikuwa ni miongoni mwa maandamano kadhaa ambayo yalipangwa kote Ufaransa kufuatia wito wa Hamas, kundi la Wapalestina linalodhibiti Gaza, kwa maandamano katika ulimwengu wa Kiislamu, Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin aliamuru maafisa wa eneo hilo kupiga marufuku maandamano yote ya Wapalestina, akitaja hatari ya machafuko ya umma.

Jinsi Vyombo vya Habari vya UU Vinavyopotosha Habari za Palestina, Uchambuzi

Ufaransa ina idadi kubwa ya Waislamu na Wayahudi, na migogoro katika Mashariki ya Kati mara nyingi huzua mivutano kati ya jumuiya hizo mbili, Darmanin alisema kuwa serikali imeongeza hatua za usalama kwa maeneo ya Wayahudi, kama vile shule na masinagogi.

Uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa utawala wa Israel unakuja wakati Ukanda wa Gaza ukilengwa na maelfu ya mabomu ya Israel tangu Jumamosi, Mashambulizi hayo ya anga yamesababisha vifo vya Wapalestina 1,500 wakiwemo watoto 500 na wanawake 280 na kuwaacha wengine zaidi ya 5,000 kujeruhiwa. Utawala huo pia umepunguza maji, chakula, mafuta na usambazaji wa umeme katika eneo hilo lililozingirwa, na kuibua wasiwasi wa kimataifa juu ya mzozo mkubwa wa kibinadamu huko Gaza.

Meya wa New York alaumiwa kwa kuwaita waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina 'Wana msimamo mkali.

Shambulio hilo la Israel limekuja baada ya harakati ya muqawama ya Hamas kuanzisha mashambulizi ya pande nyingi na ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu siku ya Jumamosi katika kile ilichokitaja kuwa Operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa, Ilisema operesheni hiyo ni jibu la kudhalilishwa kwa Msikiti wa al-Aqsa, kuongezeka kwa ghasia dhidi ya Wapalestina na uhalifu wa kukalia kwa mabavu.

 

3485555

 

 

Kishikizo: sweden qurani
captcha