Video hiyo ilionyesha ImamuSubhu akiwa amesujudu pamoja na waumini kwenye Masjid ya Al-Ula Jami, lakini hakuinuka tena na baada ya muda mfupi akatangazwa kuwa amefariki.
Muadhini, ambaye alikuwa amesimama nyuma ya imamu, aliona hali yake na akachukua jukumu la kuendeleza kusalisha maamuma. Wengi katika mitandao ya kijamii wamesema imamu huyo amepata mwisho mwema katika maisha yake ya hapa duniani.