IQNA

Mjadala wa #tilljannah (Hadi Jannah) wawavutia wanawake Waislamu

21:19 - September 25, 2016
Habari ID: 3470579
Mjadala wa #tilljannah (hadi Jannah) maalumu kwa vijana wa kike Waislamu, umefanyika pembizoni mwa Mkutano wa Kilele wa Wanawake Waislamu mwaka 2016 huko Kuala Lumpur, Malaysia na kuwavutia washiriki takribani 500.

Mkurugenzi wa mjadala huo, Saidul Redza Mohammad aliongoza mjadala kuhusu wanawake wote Waislamu katika mkutano huo ambao pia ulikuwa na maonyesho kuhusu mafanikio mbali mbali ya wanawake Waislamu.

"Mjadala huo wa siku tatu ulilengwa kuwawezesha wanawake Waislamu na tuliona vijana wa kike Waislamu wakiwa wamevutiwa sana na yaliyojadiliwa," amesema.

Saifula Reda, ambaye ni mshauri nasaha katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu Malaysia amesema wanawake mashuhuri Waislamu wakiwemo MizzNina, Fynn Jamal, na Diana Amir walishiriki katika siku ya pili ya mjadala huo ambapo walifafanua kuhusu mwamko wa kiroho waliopata.

Mkutano huo wa siku tatu ulianza Ijumaa na kumalizika Jumatatu hii ambapo kulijadiliwa maudhui kadhaa kama vile nafasi ya wanawake katika kuleta Amani, kuwawezesha wanawake Waislamu kibiashara mbali na tamasha la utamaduni wa Kiislamu.

3461003/

captcha