IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu: An-Nisa

Surah An-Nisa inaashiria umuhimu wanawake katika Qur'ani Tukufu

20:30 - January 13, 2024
Habari ID: 3478193
IQNA – Surah An-Nisa, sura ya nne ya Quran, inaanza kwa kupendekeza Taqwa (kumcha Mungu).

Kutokana na masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake yaliyotajwa katika Sura hii, imeitwa An-Nisa (wanawake), ambayo pia inaonyesha hadhi na umuhimu mkubwa wa wanawake katika Qur'ani Tukufu.

Surah An-Nisa, iliyoteremshwa Madina, ina aya 176 na iko katika Juzuu za 4 hadi 6 za Qur'ani Tukufu. Ni Sura ya 92 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Yafuatayo ni baadhi ya masuala yaliyotajwa katika Surat An-Nisaa:

  • Kuwalingania watu kumwamini Mwenyezi Mungu, uadilifu na kukata urafiki na maadui (wa Mungu).
  • Kuashiria hadithi za watu wa zamani na hatima ya jamii za mwanadamu.
  • Kusisitiza umuhimu wa kuwasaidia wenye shida wakiwemo mayatima.
  • Kufafanua juu ya sheria ya mirathi kwa kuzingatia njia ya asili na ya haki.
  • Kubainisha sheria kuhusu ndoa na mipango ya kudumisha utakasifu katika jamii.
  • Kutoa sheria za jumla kuhusu kulinda mali za jamii
  • Kuwatambulisha maadui wa jamii ya Kiislamu na kuwaonya Waislamu kuwa macho kuhusu maadui hao.
  • Kusisitiza umuhimu wa utawala wa Kiislamu na haja ya kumtii kiongozi wa serikali ya Kiislamu.
  • Kubainisha umuhimu wa Hijra (kuhama) na kadhia ambazo ni lazima.

Kuna Hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kuhusu ubora wa kusoma Surah An-Nisa. Mtume (SAW) amesema mwenye kusoma Surah An-Nisa atakuwa kama ametoa pesa kwenye njia ya Mwenyezi Mungu sawa na kiasi anachorithi Muislamu kutokana na maudhui ya Sura na atapewa ujira wa kumwacha huru mtumwa.

Ni wazi kuwa Hadithi hii na zinazofanana na hizo sio tu zinahimiza kuhusu kusoma aya, bali pia kuzitafakari na kuzifanyia kazi katika maisha ya mtu binafsi na ya kijamii.

3486783

captcha