IQNA

Watu wa Iran waandamana kuwaunga mkono wa Yemen wanaodhulumiwa

18:43 - January 28, 2022
Habari ID: 3474861
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya wananchi katika miji mingi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameshiriki katika maandamano ya kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Yemen na kulaani jinai zinazotendwa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia dhidi ya taifa hilo.

Mjini Tehran baada ya Sala ya Ijumaa katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA, maelfu ya waumini walishiriki katika maadamano ya kuunga mkono taifa la Palestina.

Waandamanaji walisikika wakitoa nara kama vile 'Mauti kwa Marekani'. 'Mauti kwa Wazayuni na Mawahabi Waibua Fitina Kubwa'. 'Mauti kwa Aal Saud', na "Kimya Mbele ya Jinai ni Khiana'. Aidha waanamanaji walitoa nara ya kuunga mkono taifa la Yemen kwa kusema 'Salamu kwa Watu wa Yemen'. 

Hivi karibuni maeneo ya makazi ya raia nchiniyanalengwa zaidi kwa mashambulizi makali ya anga ya ndege za kivita za Saudia ambapo mamia ya raia wameuawa au kujeruhiwa, wengi wakiwa ni wanawaka na watoto. Jumanne iliyopita ndege za kivita za Saudia zililenga mkoa wa kaskazini mwa Yemen wa Sa'ada na kuua watu 91. Watu wengine wasiopungua 236 walijeruhiwa. Waziri wa Afya wa Yemen Al-Mutawakil amesema muungano wa vita unaoongozwa na Saudia unalenga waziwazi raia wasio na hatia na kuwaua kwa makusudi. 

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesisitiza kuwa, mauaji ya jela ya Saada nchini Yemen yalitekelezwa kwa silaha za Marekani kufuatia mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudi Arabia.

Ripoti hiyo imesema: Muungano vamizi wa Saudia ulifanya mashambulizi makubwa ya anga kaskazini mwa Yemen, ikiwa ni pamoja na katika mji wa Sana'a, katika wiki iliyopita, na kuua makumi ya raia na kuharibu miundombinu na vituo vya huduma za kijamii."

Marekani na utawala haramu wa Israel ni washirika wakuu wa Saudi Arabia na Imarati katika vita dhidi ya taifa la Yemen. 

4031941

captcha