Katika
taarifa, Waziri wa Waqfu Misri Sheikh Mukhtar Gomaa ametoa agizo la kuasisiwa Baraza Kuu la Qur'ani Misri
ambalo limetajwa kuwa na malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na: "Kustawisha kiwango cha
kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu", "Kubuni Sera na Mpango Maalumu
wa Kuimarisha Shule za Qur'ani", na
"Kulinda Utamaduni wa Kiislamu katika Sekta ya Elimu".
Aidha baraza hilo litakuwa na majukumu mengine kama vile kuimarisha utafiti unaohusiana na qiraa ya Qur'ani Tukufu na kuhimiza harakati za Qur'ani kwa kuandaa mashindano ya Qur'ani.
Sheikh Gomaa ameongeza kuwa, mwenyekiti wa baraza hilo atakuwa ni waziri wa Waqfu huku likiwa na wanachama wasiopungua 7 na wasiozidi 15.
Misri ni mashuhuri duniani kwa wasomaji au quraa bora wa Qur'ani huku Waislamu wengi wakiwa wanavutiwa sana na Ustadh Abdul Basit Abdul Samad.