IQNA – Msikiti wa Al-Ghamama ni msikiti uliopo Madina ambapo Mtume Mtukufu (SAW) aliomba dua ya mvua. Mtume Muhammad (SAW) aliswali swala ya mvua mahali hapa wakati wa ukame. Kabla ya kumaliza swala lake mawingu yalijitokeza na mvua ikaanza kunyesha. Kwa hivyo, mahali hapa pakaitwa Ghamama, yaani “mawingu.” Mtume Mwenyezi Mungu, Muhammad (SAW) pia aliongoza swala mbili za Eid al-Fitr na Eid al-Adha katika msikiti huu.