Kwa mujibu wa televisheni ya Saudia, hii itakuwa mara ya kwanza kwa swala za jamaa za kila siku kuswaliwa katika msikiti huo mtakatifu zaidi katika Uislamu baada ya kufungwa kwa takribani miezi saba kutokana na janga la corona.
Mapema mwezi huu Saudia iliwaruhusu raia wake na wakaazi wan chi hiyo kutekeleza ibada ya Umrah mjini Makka na pia kufanya ziyara katika Msikiti wa Mtume SAW (Al-Masjid an-NabawI) katika mji wa Madina.
Idadi ya walioambukizwa corona nchini Saudia ni zaidi ya 342,000 huku waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo wakiwa zaidi ya 5,100.