IQNA

Sharti la msamaha kwa mwenye kufanya makosa na dhambi

11:56 - May 09, 2022
Habari ID: 3475225
TEHRAN (IQNA) - Njia ya maisha ya mwanadamu imepambwa kwa hadaa na vishawishi mbalimbali vya kumdanganya mwanadamu; masuala haya ya hadaa hufanya iwe vigumu kwa wanadamu kufikia malengo halali aliyojiwekea maishani.

Mwanadamu daima hujaribiwa, na kwa sababu hii anaweza kufanya mambo mabaya na kukengeuka kutoka kwenye njia sahihi.

Wakati fulani mtu hujutia dhambi aliyoifanya na kutafuta njia ya kurejea; Hii inaonyesha kwamba mwanadamu ana dhati safi au iliyotakasika kimaumbile, na kwa sababu hii, ikiwa atafanya makosa, hutafuta njia sahihi na kurekebisha kosa na kujikwamua kutoka katika kinamasi cha uchafu.

Mungu ametoa njia ya kurudi kwa mwanadamu, lakini sio wanadamu wote wanaofaulu kuwa kwenye njia hii, kwa sababu wakati mwingine makosa hupelekea mwanadamu kughafilika na kuwa mbali na Mola Muumba.

Jina la njia hii ni toba au tawba. Toba maana yake ni kurudi; Kurudi kwa Mungu. Kurudi huku kunawezekana wakati wowote na katika hatua yoyote ya makosa na dhambi. Bila shaka, kadiri unavyorudi haraka kwenye njia sahihi, inakuwa rahisi zaidi kufika hatua daraja ya juu yaaucha Mungu.

Lakini si kila kauli inaweza kuitwa kuwa ni toba; Kwa sababu toba ina hatua na masharti; Moja ya masharti yake ni kwamba mwanadamu atubu na kusisitiza juu ya toba yake sambamba na kuwa na azma na nia  ya kutorejea tena kwenye makosa na madhambi.

Sheikh Mohsen Qaraati anafananisha toba ya kweli na kuendesha gari kwa njia sahihi; Dereva anapaswa kuwa mwangalifu kuhusu makosa yake na achukue uamuzi sahihi wakati unaofaa iwapo atakuwa amefanya kosa ili kuepusha maafa.

Toba maana yake ni kuachana na makosa na kufidia makosa yaliyopita; ni kwa msingi huu ndio Mwenyezi Mungu anakubali toba: Katika aya ya 104 ya Surat At Tawbah Mwenyezi Mungu SWT anasema:

 Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

Aidha katika sehemu ya  aya ya 222 ya SSura Al-Baqarah Mwenyezi Mungu anasema

"Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha." 

Halikadhalika katika Sura ya 160 ya Sura Al Baqarah tunasoma hivi: " Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu."

Toba lazima iwe ni ya haraka, kwa sababu dhambi zikijikusanya, toba inakuwa ngumu. Ni kama vumbi kwenye nguo ambayo huondolewa kwa kupuliza, lakini uchafu  ukiwa ni ni mwingi, hauwezi kuondolewa kwa kupuliza.

captcha