IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 26

Kwa nini mwanadamu daima anakumbwa na masaibu?

17:40 - October 24, 2022
Habari ID: 3475986
TEHRAN (IQNA) – Mwanadamu hupatwa na masaibu au matatizo mbalimbali katika maisha yake yote, utotoni, akiwa mtu mzima, na anapoolewa na kuwa na familia yake.

Qur'ani Tukufu inasisitiza kwamba wanadamu wanaishi katika dhiki na shida. Lakini ugumu huu ni wa nini?

Tunasoma katika aya ya 4 ya Sura Al-Balad: “ Hakika tumemuumba mtu katika taabu.”

Kwa kuzingatia aya hii, mwanadamu ameumbwa kuwa katika shida na mateso. Ulimwengu huu ni mahali penye dhiki na masaibu.

Katika tafsiri ya Qur'ani  wa Al-Mizan, Allamah Tabatabai anasema aya hii inatuambia kwamba dhiki na matatizo yanatuzunguka katika nyanja zote za maisha yetu.

Mwanadamu anapofuata kila baraka, anaitafuta safi na isiyo na ugumu wowote. Lakini ulimwengu hauko hivyo. Katika ulimwengu huu, tunapata kila kitu kwa kiasi fulani cha ugumu. Kwa mfano, ikiwa tunataka kula kitu, tunahitaji kutumia wakati kupika chakula. Ili kupumzika sehemu nzuri, tunahitaji kufanya kazi kwa bidii ili tupate pesa za kununua au kukodisha nyumba. Kila jambo tunalotimiza limefanikiwa kwa ugumu mwingi na hata baada ya kufikiwa, lina kila aina ya mapungufu.

Huenda tukafikiri kwamba baadhi ya watu hawakabili shida na matatizo maishani kwa sababu wao ni matajiri na wana kila kitu wanachohitaji. Lakini sivyo ilivyo hata kidogo. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa masiabu, mateso na ugumu.

Furaha kamili haiwezi kupatikana katika ulimwengu huu. Tunaweza kupata uzoefu katika ulimwengu ujao. Faraja, amani na furaha zinazotungoja huko Akhera zinafanya dhiki na mateso hapa duniani kuwa ya kustahimilika.

Kwa maneno mengine, inaweza kusemwa kwamba taabu na matatizo tunayokabiliana nayo katika ulimwengu huu ndiyo tunayolipa ili kufikia furaha inayotungoja katika ulimwengu ujao. Tab'an maisha bora katika akhera yatategemea amali zetu njema ambazo tutatenda duniani pamoja na kuwa tunakabiliwa na masaibu.

Habari zinazohusiana
captcha