IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu

Qari maarufu kijana kutoka Oman akiwa anasoma Qur'ani katika Sala ya Jamaa (+Video)

13:35 - December 22, 2022
Habari ID: 3476289
TEHRAN (IQNA) – Osama al-Zahri al-Balushi, ni qari kijana huko Oman, na qiraa yake ya Qur'ani Tukufu katika sala ya jamaa imesambaa katika mitandao ya kijamii.

Klipi ya qiraa yake iliyo hapa chini ni  katika Msikiti wa Abu Hanifa wakati wa sala ya Tarawih ambayo ni Sala maalumu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika klipu hii Al-Balushi anasoma aya za 190 hadi 195 za Sura Al Imran katika Qur'ani Tukufu.

"Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio dhulumu hawana wasaidizi. Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema. Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi. Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi. Basi walio hama, na walio tolewa makwao, na wakateswa katika Njia yangu, na wakapigana, na wakauliwa, kwa yakini Mimi nitawafutia makosa yao, na kwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayo pita mito kati yake. Hayo ndiyo malipo yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kwake yapo malipo mema kabisa."

 

3481781

captcha