IQNA

Mwanazuoni Ampongeza Sheikh Zakzaky kwa Kuinua Bendera ya Uislamu Barani Afrika

13:05 - October 18, 2023
Habari ID: 3477752
TEHRAN (IQNA) - Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) katika mji wa Mashhad Kaskazini Mashariki mwa Iran alimkaribisha Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kufanya mazungumzo naye siku ya Jumatatu.

Hujjat-al-Islamu Ahmad Marvi alikutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky mjini Mashhad, Mwanaharakati  huyo wa Nigeria na mkewe waliwasili katika mji wa kaskazini mashariki mwa Iran siku ya Jumapili.

Wakati wa mkutano uliofanyika katika eneo la Haram ya Imam Ridha (AS), Marvi alimsifu Zakzaky kama kielelezo mashuhuri cha kuigwa kwa wanaharakati wa kidini.

Pia alisifu nafasi ya kipaji ya Sheikh Zakzaky katika "kuwaongoza watu wa Kiafrika kwenye hali ya kiroho, na maadili ya Mwenyezi mungu na ya kibinadamu.

Akiyaita motisha, mapambano, uhodari, na upinzani wa mwanaharakati wa Kiafrika kuwa kifani kwa wanaharakati  wote wa kidini, mkuu wa kanisa hilo alisema, Mmeinua bendera ya Jihadi, Uislamu na umoja wa Waislamu katika Afrika.

Sheikh Zakzaky, kwa upande wake, alishukuru mapokezi mazuri ya Imam Ridha, akisema, Asante Mwenyezi Mungu, nimebarikiwa  kufanya Ziyara kwenye eneo hili takatifu, ambalo ni kimbilio la amani kwa kila mtu.

Maafa ya kibinadamu huko Gaza

Katika sehemu nyingine, Marvi ameashiria zaidi matukio ya hivi karibuni ya Palestina na kusema, Maafa ya kibinadamu huko Gaza dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina mikononi mwa utawala ghasibu wa Israel kiuhalisia ni jinai dhidi ya ubinadamu, jambo ambalo linaumiza moyo mtu yeyote bila ya kujali taifa, kabila na imani.

Matamshi hayo yanajiri katika hali ambayo utawala haramu wa Israel umekuwa ukiushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza tangu Jumamosi iliyopita, baada ya kuanzishwa Operesheni ya Kimbunga cha  Al-Aqsa na makundi ya muqawama ya Palestina ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi 1,000 na walowezi wa Israel.

Mashambulizi hayo ya Israel yamegharimu maisha ya zaidi ya Wapalestina 2,800, wakiwemo watoto wasiopungua 1,000. Zaidi ya wakazi milioni moja wa kaskazini mwa Gaza wameyakimbia makazi yao na kuhamishwa kuelekea kusini baada ya utawala unaokalia kwa mabavu kutoa onyo kuhusu uwezekano wa uvamizi wa ardhini katika eneo hilo.

Akisisitiza kwamba ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina unaungwa mkono na Marekani na nchi za Ulaya, mlinzi huyo aliendelea kusema, Kimya kuelekea mauaji ya halaiki ya Wapalestina, na kuzingirwa haramu kwa Ukanda wa Gaza ni mbaya sana kana kwamba dhamiri ya binadamu imekufa.

Haji Marvi alihitimisha matamshi yake kwa kurejelea aya ya Qur’ani  Tukufu na kuongeza, Tuna matumaini kwamba harakati ya uadilifu ya Uislamu safi itashinda Jinai za kichaa za Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi zinaashiria kukata tamaa na woga wao huku wakijiona wako kwenye hatihati ya kuangamizwa.

 

3485623

 

Kishikizo: imam ridha zakzaky
captcha