IQNA

Malaika

Malaika Ni Nani?

23:01 - January 08, 2024
Habari ID: 3478169
IQNA - Malaika ni viumbe vya mbinguni ambavyo vimeumbwa kutokana na nuru na imani ya kuwepo kwao ni jambo la lazima kwa Waislamu.

Malaika hawaonekani na hawawezi kuonekana kwa macho yetu. Jibreel (Gabriel), Mikaeel, Israfil na Izra’il ni malaika wakuu wanne ambao majina yao yametajwa katika Qur’ani Tukufu.

Qur’ani Tukufu pia inawataja baadhi ya malaika wengine, wakiwemo Harut, Marut, Nakir na Munkar.

Hizi ni baadhi ya sifa za Malaika kwa mujibu wa aya za Qur’ani Tukufu:

1- Wanamtii Mungu na kamwe hawatendi dhambi.

“Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.” (Aya ya 27 ya Surat Al-Anbiya)

2- Wana majukumu muhimu na tofauti tofauti:

“Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi”. (Aya ya 17 ya Surah Al-Haqqa)

"...na kwa (Malaika) wanaosimamia mambo." (Aya ya 5 ya Surah An-Nazi’at)

“Hao itawafikia sehemu yao waliyo andikiwa, mpaka watakapo wafikia wajumbe wetu(Malaika) kuwafisha, watawaambia: Wako wapi mlio kuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? …” (Aya ya 37 ya Surat Al-A’raf)

“… Na hakika bila ya shaka wapo walinzi (Malaika) juu yenu, Waandishi wenye hishima, Wanayajua mnayo yatenda. Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema. (Aya ya 10-13 ya Surah Al-Infitar)

“Na hukupelekeeni waangalizi (Malaika), mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.…” (Aya ya 61 ya Surat Al-An’am).

Baadhi yao wamepewa jukumu la kutoa adhabu (Aya ya 77 ya Surah Hud). Wengine huwasaidia Waumini katika vita (Aya ya 9 ya Surah Al-Ahzab). Na wengine huleta vitabu vya Mwenyezi Mungu kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu (Aya ya 2 ya Surat An-Nahl)

3- Wanamuabudu Mwenyezi Mungu daima: “… (Aya ya 5 ya Sura Ash-Shura)

4- Wakati fulani huwatokea manabii au wengine kwa sura ya wanadamu.

"Tulimpelekea Roho Wetu (Jibril) kama mtu mkamilifu." (Aya ya 17 ya Surat Maryam)

Soma zaidi:

5- Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.  Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.  Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa. ( As Saffat Aya ya 164-166)

Katika Aya ya 285 ya Sura Al-Baqarah, Mwenyezi Mungu anasisitiza umuhimu wa kuwaamini Malaika: “Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake.”

Kishikizo: malaika al jinn
captcha