IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Algeria watunukiwa

21:41 - February 10, 2024
Habari ID: 3478330
Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Algeria watunukiwa IQNA –Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Algeria yalihitimishwa siku ya Ijumaa.

Washindi wa walitajwa na kutunukiwa zawadi katika hafla ya kufunga mashindano hayo, iliripoti al-Wasat.

Jopo la majaji lilimtambulisha Ahmed al-Alam mwenye umri wa miaka 23 kutoka Libya kama mshindi wa kwanza akifuatiwa na Yusuf Abdul Rahman kutoka nchi mwenyeji na wa tatu ni Ahmad al-Bashir kutoka Bangladesh.

Wajumbe wa jopo la majaji akiwemo Taqi al-Deen kutoka Palestina na Sheikh Islam bin Fouzi Dashkin kutoka Russia pia walitunukiwa zawadi katika sherehe za kufunga zilizohudhuriwa na baadhi ya maafisa wakuu wa kisiasa na kidini wa Algeria.

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Algeria huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya nchi hiyo.

Wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 40 walishiriki katika mashindano hayo mwaka huu.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

3487135

captcha