IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Morocco ashika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Bahrain

17:09 - April 25, 2024
Habari ID: 3478732
IQNA - Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani ya Bahrain yalihitimishwa Jumatano usiku.

Washindi wa tukio la Qur'ani walitajwa na kutunukiwa zawadi katika hafla ya kufunga ambapo El-Yas Hajri kutoka Morocco alishinda tuzo ya juu katika kategoria kuu, ya kuhifadhi Qur'ani.
Mwananchi mwenzake Yaseen al-Kazini alishika nafasi ya pili. Katika usomaji wa Tajweed, Muhammad Sameer Mujahid kutoka nchi mwenyeji alinyakua zawadi ya kwanza. Na katika kategoria ya usomaji wa Qur'ani kwa watoto, Ahmed Muhammad Salih Ahmed kutoka Yemen aliongoza.
Mashindano hayo yalifanyika kwanza kwanza kupitia intaneti katika na washindi wa mchujo huo walishiriki katika mashindano ya ana kwa ana katika fainali.
Zaidi ya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani 5,000 kutoka nchi 74 walishindana katika hatua ya mchujo.
Waandaji wanasema mashindano hayo yanalenga kuhudumia Qur'ani Tukufu na kuwahimiza Waislamu kusoma na kuhifadhi Kitabu Hicho Kitukufu.

 

 

 

 
 

4212309

captcha