IQNA

Zaidi ya nchi 62 kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Iran

15:43 - April 21, 2015
Habari ID: 3185599
Zaidi ya nchi 62 zimethibitisha kushiriki katika awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi alipozungumza na waandishi habari jana Jumatatu mjini Tehran. Ameongeza kuwa mashindano ya mwaka jana yalikuwa na washiriki kutoka nchi 70 na kwamba mwaka huu idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka. Sheikh Ali Mohammad amesisitiza kuwa kushiriki kwa wingi wawakilishi wa nchi mbali mbali duniani ni isharakuwa, kinyume na madai ya maadui, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijatengwa kimataifa. Aidha amesisitza kuhusu umuhimu wa kueneza ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu kupitia mashindano hayo.
Awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuanza katika mji mkuu Tehran mnamo 27 Rajab sawa na Mei 15.
Mashindano hayo yataanza sanjari na mnasaba wa Mab’ath (kubaathiwa  au kupewa utume Mtume Muhammad SAW).  Mashindano hayo ya kila mwaka yataendelea kwa muda wa wiki moja hadi Ijumaa tarehe 22 Mei.
Wasomi (maqarii) na waliohifadhi Qur’ani kikamilifu kutoka nchi za Kiislamu na zisizo na Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo ya wiki moja. Hassan Danesh ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kitengo cha qiraa au kusoma huku Mohammad Mehdi Rajabi akishiriki katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu…/EM

3183388

captcha