IQNA

Mikono iliyofungwa ya shetani katika mwezi wa Ramadhani

19:54 - April 25, 2022
Habari ID: 3475169
TEHRAN (IQNA)- Moja ya mambo ambayo yamesemwa kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwamba mkono wa shetani umefungwa ndani ya mwezi huu.

 Lakini ikiwa shetani yuko katika kikomo, je, hiyo ina maana kwamba hakuna mtu anayeweza kujaribiwa au kufanya makosa mwezi huu?

Katika khutba ya Sha'baniyah, Mtume wa Uislamu (SAW) alieleza sifa za mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema katika sehemu yake: "Na Mashetani wamefungwa, hivyo Muombe Mungu asiwaache wakutawale." Masuala mawili yametolewa kutoka katika sehemu hii ya Dua ya Sha'baniyah; Kwanza, mashetani huzuiliwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani; Lakini jambo la pili linaonyesha kwamba wakati huo huo, shetani anaweza kuwatawala watu wanaofunga.

Qur’ani inamuonyesha shetani kuwa ni dhaifu sana na inasisitiza kwamba shetani na wasaidizi  wake hawana mamlaka juu ya waja wa Mungu; Kwa sababu Mungu, katika kujibu vitisho vya shetani vya kuwapotosha waja wakei, alizungumza juu ya ukosefu wake wa utawala na alitangaza tu utawala wa shetani uko tu juu ya wale wanaomfuata. Utawala uliotajwa katika hapo juu pia unamaanisha ushawishi mkubwa.

Ramadhani ni wakati muhimu wa kujiimarisha kiroho. Ni mwezi ambao imeteremshwa ndani yake Qur’ani ; Usiku wa kudra umo ndani yake; Ibada ni tofauti katika mwezi huo, kama vile kupumua na usingizi wa Muumini ni ibada; Usomaji wa aya moja ya Qur'ani ni sawa na usomaji wa Qur'ani nzima. Kwa sababu hii, shetani hawezi kupenya mioyo ya watu waliofunga ambao wanamwabudu na kumkumbuka Mungu kila wakati katika mwezi huu.

Kwa maana hiyo nyoyo za watu waliofunga huwa zimejawa na nuru na kumkumbuka Mwenyezi Mungu kutokana na kufunga kwao na kuwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kutekeleza amali za mwezi huu mtukufu, na  hivyo shetani anasalimu amri kwa moyo huo. Hivyo, mfungaji asipojijenga na kumkumbuka Mungu katika siku hizi, nuru ya moyo wake itakuwa dhaifu na njia itatayarishwa kwa ushawishi wa shetani.

Kama inavyosisitizwa ndani ya Qur’ani Tukufu katika aya ya 36 ya Suuratul Azzukhruf kwamba “Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea shetani kuwa ndiye rafiki yake.”

Kwa upande mwingine, imepokewa kwamba Mtume wa Muhammad SAW amesema: "Hakika shetani hutiririka ndani ya mwanadamu kama mtiririko wa damu, kwa hivyo jizuie kula ili uifanye njia yake iwe panda.”

Kwa hivyo kukula chakula kichache, kujizuia kula na saumu  hufunga njia ya shetani kujipenyeza katika moyo wa mwanadamu. Ni kwa sababu hii ndiyo sababu inashauriwa kula kidogo na kufunga mara kwa mara katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani.

Kishikizo: ramadhani shetani
captcha