IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Maana ya Ramadhani

18:13 - March 16, 2024
Habari ID: 3478523
IQNA-Neno Ramadhani linatokana na mzizi wa "Ra Ma Dha" na muundo wake wa wingi ni Ramadanat na Armidha. Maana yake ni joto kali na inasemekana Waarabu walipotaka kuitaja miezi ya mwaka, mwezi huu waliupa jina la Ramadhani kwa sababu wakati huo ilikuwa katika kipindi cha mwaka ambapo hali ya hewa ilikuwa ya joto sana.

Lakini baadhi ya wafasiri wa Qur’ani kama Tabari, wanapofasiri Aya ya 185 ya Surah Al-Baqarah, “Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi...”, wamemnukuu Mujahid bin Jabar akisema kuwa Ramadhani inaelekea kuwa ni miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu na haihusiani na joto kali.

Pia kuna maoni mengine kuhusu jina la Ramadhani, huku wengine wakisema linatoka kwa Ramada as-Sa’im, kumaanisha wakati ambapo mfungaji anahisi joto katika mwili wake kutokana na kiu kali. Wengine wanasema Ramadhani inatoka kwa Armadh, ambayo ina maana ya kushika moto, kama dhambi zinawaka na kuharibiwa na matendo mema.

Wengine wanasema Ramadhani inatokana na Ramadha, ambayo ina maana ya jiwe la moto, huku mioyo ikiyeyuka kwa kutafakari akhera.

Wengine wanasema inatoka kwa Ramdhat an-Nasl, ambayo ina maana ya kunoa upanga, kwani Waarabu walinoa panga zao katika Ramadhani ili kwenda vitani kabla ya miezi ya Haram (wakati vita vilikatazwa).

Katika zama za Jahiliyah (kabla ya kuja Uislamu) mwezi huu uliitwa Natiq na Waarabu waliuheshimu. Watu wa Thamud waliiita Dimmir na mwaka wao ulianza na mwezi huu.

3487543

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ramadhani
captcha