IQNA

Qur'ani Tukufu katika Mwezi wa Ramadhani

Juhudi za kuboresha kipindi cha Qur'ani cha Televisheni cha 'Mahfel'

21:34 - March 12, 2024
Habari ID: 3478494
IQNA - Timu inayohusika katika utayarishaji wa "Mahfel", kipindi cha Televishecni cha Qur’ani cha Ramadhani nchini, imefanya juhudi za kuimarisha ubora wa kipindi hicho kat ika msimu wake wa pili.

Msimu wa pili wa kipindi maalum cha "Mahfel" unapamba skrini za chaneli ya 3 ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kabla ya adhana ya Magharibi, na kuwapa watazamaji hali nzuri ya kimaanawi wanapojitayarisha kufuturu.

Haya ni kwa mujibu wa Resalat Buzari, mtangazaji wa kipindi hicho, ambaye alisema kuwa watazamaji walikaribisha vipindi hivyo katika msimu wa kwanza, jambo ambalo liliwafanya watayarishaji kuzingatia zaidi kuboresha ubora wa kipindi hicho.

Kipindi hicho ambacho kimelenga zaidi kuangazia ujuzi wa Qur'ani kinatoa fursa kwa watu walio katika saumu kusikiliza mijadala yenye mafundisho pamoja na usomaji wa Qur'ani wenye mvuto.

Kipengele muhimu kinachochangia mvuto wa programu hiyo ni kujumuishwa kwa wataalamu wa Qur'ani, hasa wasomi mashuhuri wa kigeni kama vile Sayyid Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq na Rizwan Darwish kutoka Syria. Programu hiyo pia ina wataalam wawili wa Iran, ambao ni qaris mashuhuri Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi.

Buzari aliiambia IQNA kwamba watazamaji sasa wana matarajio makubwa kutoka kwa programu baada ya mafanikio ya mfululizo wa kwanza.

3487532

Habari zinazohusiana
captcha