IQNA

Mwezi wa Ramadhani

WHO yatoa ushauri kuhusu kufunga Kiafya Wakati wa Mwezi wa Ramadhani

22:27 - March 19, 2023
Habari ID: 3476732
TEHRAN (IQNA) – Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatarajiwa kuanza wiki ijayo na Waislamu duniani wanasubiri kwa hamu kubwa kuanza kufunga katika mwezi huo mtukufu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa ushauri kuhusu kufunga kwa afya katika mwezi wa Ramadhani, kuanzia kujiepusha na vitafunio vyenye sukari tele hadi ulaji wa matunda na mboga.

Hapa kuna mambo machache ya kuzingatia kuhusu kufunga wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kulingana na WHO:

Wakati maalum wa mwaka umekaribia. Tamasha kubwa zaidi la jamii ya Kiislamu limepangwa kusherehekewa. Mwezi mtukufu wa Ramadhani wa kalenda ya Kiislamu huzingatiwa na Waislamu kuanzia  Alfajiri hadi Magharibi. Waislamu huanza saumu kabla ya Sala ya Alfajiri, na kisha wakafungua baada ya kuzama kwa jua. Kwa kawaida kufuturu ni huanza kwa tende tatu na maji na kisha vyakula mbali mbali.

Mwaka huu, Ramadhani inatazamiwa kuanza Machi 22 au 23 na itamalizika Aprili 21, kwa kutegemea mwezi mwandamo. Tunapojiandaa kwa ajili ya Ramadhani, hapa kuna muongozo wa Shirika la Afya Ulimwenguni kwa ajili ya afya njema mwezi mzima:

Maji ya kunywa: Saumu huanza na suhur  au daku, yaani chakula kinacholiwa kabla ya Sala ya Alfajiri  na kuishia na futari wakati wa Magharibi.

Ni vyema  tukumbuke kunywa maji mengi ili kuupa mwili virutubishi ambavyo unakosa.

Matunda: Ulaji wa matunda na mboga mboga zenye maji mengi utasaidia kuupa mwili unyevu na kuuweka ukiwa na afya.

Ni bora wakati mwingi ukae mahali penye kivuli au pasipo na joto kali.

Suhur au Daku:  Ni muhimu sana kujumuisha mboga, sehemu ya wanga na chakula chenye protini nyingi ili kuongeza nishati mwilini.

Pipi: pia inashauriwa kuepuka kutumia idadi kubwa ya vitafunio vyenye sukari tele wakatu wa futari na pia ni bora kujiepusha kula vyakula vyenye mafuta mengi.

Vyakula vya kukaanga: Inashauriwa kutumia njia nyingine za kupika kuliko kukaanga ili kuufanya mwili uwe na afya njema katika kipindi chote cha Ramadhani.

3482855

Kishikizo: ramadhani chakula
captcha