IQNA

Qur'ani Tukufu katika Mwezi wa Ramadhani

Kipindi cha Qur'ani cha Televisheni cha 'Mahfel' chavutia wengi

18:28 - March 11, 2024
Habari ID: 3478487
IQNA - Mmoja wa wataalam na majaji wa "Mahfel", kipindi cha Qur'ani kitakachorushwa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, anasema alishangazwa na ubora wa hali ya juu wa wageni katika msimu wa pili.

Msimu wa pili unaotarajiwa wa kipindi maalum cha "Mahfel" unatazamiwa kupamba skrini za chaneli ya 3 ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kabla ya adhana ya Magharibi, na kuwapa watazamaji hali nzuri ya kimaanawi wanapojitayarisha kufuturu.

Kipindi hicho ambacho kimelenga zaidi kuangazia ujuzi wa Qur'ani kinatoa fursa kwa watu walio katika saumu kusikiliza mijadala yenye mafundisho pamoja na usomaji wa Qur'ani wenye mvuto.

Jambo muhimu linalochangia mvuto wa programu hiyo ni kujumuishwa kwa wataalamu wa Qur'ani, hasa wasomi mashuhuri wa kigeni kama vile Sayyid Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq na Rizwan Darwish kutoka Syria. Programu hiyo pia ina wataalam wawili wa Iran, ambao ni maqari mashuhuri Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi.

Akizungumza na IQNA, al-Hulw alisema kuwa timu nzima ya "Mahfel" inalenga kuwavutia "watazamaji mara kadhaa zaidi" kwa msimu wake wa pili ikilinganishwa na wa kwanza.

Baadhi ya watu walipendekeza, baada ya msimu wa kwanza kumalizika, kwamba walitaka onyesho liendelee mwaka mzima, labda kila wiki au mwezi, aliongeza.

Kulingana na takwimu za hivi punde zaidi ya Wairani milioni 30 walitazama  "Mahfel," al-Hulw alisema, na kuongeza, "Zaidi ya hayo, tulikuwa na watazamaji kutoka nchi za kigeni, hasa kutoka mataifa ya Kiarabu, lakini pia kutoka nchi zisizozungumza Kiarabu kama vileUfilipino, Indonesia, na Malaysia.”

3487507

Habari zinazohusiana
captcha