IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Mwimbaji wa Korea asema alisilimu baada ya kuvutiwa na Qur’ani

17:58 - March 16, 2024
Habari ID: 3478522
IQNA - Daud Kim, mwimbaji maarufu wa pop wa Korea Kusini na YouTuber, amesimulia namna alivyoukubali Uislamu kuwa muongozo katika maisha yake.

Kim amesimulia kisa  hicho katika kipindi maalum cha TV cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Iran.

Sehemu ya 4 ya msimu wa pili wa kipindi cha TV cha Mahfel siku ya Ijumaa kilimshirikisha Kim ambaye alikuwa ametoka Korea Kusini kuja Iran ili kusimulia kisa chake cha kusilimu kwa mamilioni ya watazamaji ambao husikiliza kipindi hicho kila siku kabla ya iftari katika mwezi wa Ramadhani.

Akibainisha kuwa Uislamu sio dini ya wengi nchini Korea, Kim alisema kuwa vyombo vya habari vinazungumza kuhusu Uislamu kwa "njia mbaya". "Nilipokuwa mdogo nilifikiri Uislamu ni jambo la hatari," amesema.

Kuwa mwanamuziki kulimpa nafasi ya kutumbuiza katika nchi nyingine na safari yake ya Indonesia ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na Waislamu, amebaini.

Kuongezeka kwa shauku yake katika Uislamu kulimfanya asome zaidi kuhusu dini alipofikarejea nyumbani, anaongeza kuwa, “hivyo nikasoma Qur’ani. Nilijaribu kuswali na kufunga.”

"Niliposoma Qur’ani, nilipata kitu ambacho kilinivutia sana," alisema, akiashiria mafundsho ya Tauhidi ambayo yamengaziwa katika Quran Tukufu.

"Kuna jambo ambalo hutufanya tuwe na furaha na amani, na madhumuni ya maisha yako katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kupitia kumtii Mwenyezi Mungu tunapata furaha ya kweli na amani ya kweli katika akili," Kim alibainisha.

Hili ndilo jambo "ambalo nilihitaji sana," alikumbusha. "Jambo ambalo hunifanya kuwa na furaha na amani."

Alibainisha kuwa baada ya utafiti hatimaya alitamka Shahada mbuli na  akawa Mwislamu.

Katika kipindi hicho cha televisheni Kim pia alisoma Surah al-Ikhlas. Kim, ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la Jay Kim, alisilimu mnamo Septemba 2019 na akatangaza kusilimu kwake kwenye video ya YouTube.

Waislamu ni wachache nchini Korea Kusini, ambao ni chini ya asilimia 1 ya watu wote. Wengi wao ni wageni, kama vile wafanyikazi wahamiaji na wanafunzi wa kimataifa. Msikiti wa kwanza nchini Korea Kusini, Msikiti wa Kati wa Seoul, ulijengwa mnamo 1976. Tangu wakati huo, misikiti 15 zaidi imesajiliwa rasmi kote nchini, pamoja na musalla 150 hadi 200, au sehemu ndogo za ibada.

Onyesho la msimu wa pili wa kipindi hicho maarufu lilianza kwenye chaneli ya 3 ya IRIB katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Jumanne.

Hutangazwa kabla ya Magharibi  kila siku katika mwezi mtukufu, na kutoa mahali pazuri pa kiroho kwa watazamaji wanapojitayarisha kufuturu.

Kipindi hicho ambacho kimelenga zaidi kuangazia ujuzi wa Qur'ani kinatoa fursa kwa watu walio katika saumu kusikiliza mijadala yenye mafundisho pamoja na usomaji wa Qur'ani wenye mvuto.

Kipengele muhimu kinachochangia mvuto wa programu hiyo ni kujumuishwa kwa wataalamu wa Qur'ani, hasa wasomi mashuhuri wa kigeni kama vile Sayyid Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq na Rizwan Darwish kutoka Syria. Programu hiyo pia ina wataalam wawili wa Iran, ambao ni maqari mashuhuri Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi.

 

3487581

 

Habari zinazohusiana
captcha