IQNA

Qur'ani Tukufu katika Mwezi wa Ramadhani

Qari wa Syria: Kipindi cha televisheni cha Mahfel huwahimiza wengi kujifunza Qur’ani

16:11 - March 15, 2024
Habari ID: 3478519
IQNA – Mtaalamu wa Qur’ani na qari wa Syria amesifu “Mahfel”, kipindi cha Televisheni cha Qur’ani kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa kuhimiza watu kujifunza Qur’ani.

Rizwan Darwish aliiambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) katika mahojiano kwamba watu wamesambaza vipindi vya programu kwenye YouTube na baada ya kuvitazama mtandaoni, wengi wamevutiwa kujifunza Kitabu Kitakatifu.

Onyesho la msimu wa pili wa kipindi hicho maarufu lilianza kwenye chaneli ya 3 ya IRIB katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Jumanne.

Hutangazwa kabla ya Magharibi  kila siku katika mwezi mtukufu, na kutoa mahali pazuri pa kiroho kwa watazamaji wanapojitayarisha kufuturu.

Kipindi hicho ambacho kimelenga zaidi kuangazia ujuzi wa Qur'ani kinatoa fursa kwa watu walio katika saumu kusikiliza mijadala yenye mafundisho pamoja na usomaji wa Qur'ani wenye mvuto.

Kipengele muhimu kinachochangia mvuto wa programu hiyo ni kujumuishwa kwa wataalamu wa Qur'ani, hasa wasomi mashuhuri wa kigeni kama vile Sayyid Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq na Rizwan Darwish kutoka Syria. Programu hiyo pia ina wataalam wawili wa Iran, ambao ni qaris mashuhuri Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi.

Darwish aliiambia IQNA kwamba vipindi vya msimu wa kwanza, ambavyo vilitangazwa wakati wa Ramadhani ya mwaka jana, vimewafanya wengi, hata wale ambao hapo awali hawakupenda shughuli za Qur'ani, kuanza kujifunza Qur'ani.

Alisema kipindi hicho cha TV ni cha kipekee katika ulimwengu wa Kiislamu na hajaona kinachofanana na hicho katika nchi nyingine.

Pia alisema washiriki wa msimu wa pili, sawa na wale wa kwanza, ni watu binafsi wenye uwezo mkubwa na ujuzi wa juu wa Qur'ani.

Qari huyo wa Syria alisisitiza zaidi kwamba kutokana na mafanikio yake makubwa na umaarufu mkubwa, kipindi hiki cha televisheni cha Qur'ani kinapaswa kuendelea kutayarishwa katika miaka ijayo kwani watu wana hamu ya kukitazama.

Alipoulizwa kama kuna haja ya kuwa na mabadiliko katika misimu ijayo, alisema kuwa, kwa kawaida, kila mtu anataka kusonga mbele kwenye njia ya maendeleo na uboreshaji na mpango huu pia unaweza kuboresha na kuwa bora zaidi kwa kuanzishwa kwa baadhi ya mabadiliko.

Alizaliwa tarehe 8 Machi 1965, huko Damascus, Darwish ni Muislamu wa Kisunni ambaye ni Msomaji wa Qur’ani na Ibtihal.

Yeye ni qari anayesifika kimataifa ambaye amewahi kuwa mjumbe wa jopo la majaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika nchi tofauti, ikiwemo Iran.

3487563

Habari zinazohusiana
captcha