IQNA

Mawaidha

Kupokea Rehema za Mungu zisizo na kikomo katika Siku za Mwisho za Ramadhani

13:40 - April 20, 2023
Habari ID: 3476891
TEHRAN (IQNA) – Katika saa hizi tunazoelekea mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie rehema zake zisizo na kikomo.

Moja ya mambo ambayo tunaweza kumuomba Mwenyezi Mungu katika nyakati hizi za mwisho za Ramadhani ni rehema ya Mwenyezi Mungu ambayo tunaweza kufurahia kwa muda wote uliobaki wa mwaka.

Katika dua iliyotengwa kwa ajili ya siku ya 29 ya Ramadhani, tunasoma: “Ee Mwenyezi Mungu! Nifunike katika mwezi huu kwa rehema, Uniruzuku uongofu na kulinda na machafu, Utahirishe moyo wangu usiingiwe na giza la shaka Ewe Mrehemevu wa waja wako walio wema.”

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atufunike kwa rehema zake kwani akitaka kumjalia mtu kitu, hakuna kinachoweza kuzuia baraka hii. Kwa upande mwingine, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kumnyima mtu rehema yake basi hakuna nguvu nyingine inayoweza kuingilia kati.

Kuchukua hatua katika kumtii Mwenyezi Mungu ni mafanikio ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu huwapa waja wake. Wanadamu hawawezi kufanya tendo lolote isipokuwa Mungu awape uwezo wa kufanya hivyo. Mungu ndiye Muumba wa viumbe vyote na ni Muweza wa kila jambo.

Kuna baadhi ya maagizo ambayo yanaweza kutusaidia kuacha dhambi; haya ni pamoja na kudhibiti macho na masikio ya mtu na kujiepusha na marafiki wabaya. Pia, ili kuondoa mawazo juu ya dhambi, mtu anaweza kuandaa mipango ya kila siku, kufunga, kufanya mazoezi, na kufikiria kifo.

Huruma ya Mungu inaweza kugawanywa katika makundi mawili: maalum na ya umma. Rehema ya umma inatolewa kwa viumbe vyote, hata wanadamu wenye dhambi; hizi ni pamoja na baraka za kuishi. Hata hivyo, rehema maalum ya Mungu ni kwa ajili ya wenye haki pekee. Rehema hii inajumuisha kuishi maisha yenye msingi wa njia ya Mungu na kufika Peponi.

Makala haya yametolewa katika kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiajemi chaHujjatul Islam Ruhollah Bidram.

Kishikizo: ramadhani MAWAIDHA
captcha