IQNA

Mawaidha

Jinsi ya kudumisha hali ya kiroho iliyopatikana Mwezi wa Ramadhani

20:33 - April 24, 2023
Habari ID: 3476909
Tehran (IQNA) - Kudumisha hali ya kiroho ambayo Mwislamu ameipata wakati wa mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani kunahitaji kutumia miongozo iliyojengeka roho ya mtu binafsi na mawaidha ya wanazuoni wa kidini.

Kudumisha na kulinda kile mtu amepata wakati wa mwezi wa kufunga wa Ramadhani ni muhimu sana. Kuna watu wachache ambao wanajaribu kuchukua hatua moja zaidi na kuinua hali yao ya kiroho hadi Ramadhani inayofuata.

Tukiangazia asili ya wanadamu, tunaweza kuona kwamba sisi ni tofauti ikilinganishwa na viumbe vingine. Malaika wana hali ya kiroho tu na wanyama wana sifa tu za kihayawani; Walakini, wanadamu wako kati kwani wana sifa hizi zote mbili.

Kwa ufupi, wanadamu wana hali ya mwili ambayo ina mahitaji yake mwenyewe na tunayo jukumu la kufuata maagizo kadhaa ya kujiweka katika hali nzuri ya siha na afya. Wakati huo huo, wanadamu wana hali ya kiroho ambayo pia inahitaji ulinzi na utunzaji. Tukiangazia dua za wanazuoni na mawalii inatubainikiwa kwamba wanamuuliza Mungu kwa afya ya miili yao na ya roho pia.

Quran Tukufu inabaini kuwa "moyo safi" ndio utakaosaidia watu katika Akhera: "  Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.  Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. (Sura Ash-Shu'araa, aya 88-89)

Vivutio vya ulimwengu vinaweza kuwafanya watu kusahau mambo ya kiroho na hivyo kuna haja ya kuwakumbusha waumini mara kwa mara kuhusu kudumisha hali ya kiroho na kimaanawi.

Wakati huo huo, ukamilifu wa mwanadamu kiroho hutegemea namna anavyoweza kuibuka mshindi mbele ya matamanio ya kidunia. Kwa hakika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kozi nzuri ya mafunzo ya kuimarisha irada ya kiroho ya Mwislamu.

Hii ni sehemu ya mahojiano ya IQNA na Mohammad Asadi Garmaroudi, profesa na mkuu wa masomo ya Kiisilamu katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif jijiniTehran.

captcha